National News

KIGOMA YAADHIMISHA MIAKA 62 YA UHURU KWA KUFANYA SHUGHULI MBALIMBALI

Tarehe: 09 Dec, 2023


Katika kuadhimisha miaka 62 ya uhuru wa Tanzania mkoani Kigoma shughuli mbalimbali zimefanyika ikiwemo kupandwa kwa miche ya kisasa ya michikichi zaidi ya 200 zoezi lililoongozwa na Mkuu wa Mkoa wa Kigoma Thobias Andengenye pamoja na zoezi la kufanya usafi katika Soko la Nazareti. 

Akizungumza na wakazi wa Mkoa wa eneo la Machinjioni Manispaa ya Kigoma Ujiji kabla ya kugawa miche hiyo Andengenye amesema kuwa kila mwananchi anajukumu la kuhakikisha anakabiliana na adui Ujinga, maradhi na umasikini pamoja na kufanya kazi kwa bidii ili kuimarisha uchumi wa mkoa na taifa kwa ujumla.

Katika hatua nyingine Andengenye amesema kuwa mkoa unajivunia mapinduzi makubwa ya miundombinu yanayoendelea kufanyika ikiwemo ujezi wa barabara mbalimbali kwa kiwango cha lami, ukarabati na upanuzi wa uwanja wa ndege, mkoa kuunganishwa na umeme wa gridi ya taifa, uboreshwaji wa miundombinu ya elimu,ujenzi wa  vyuo vikuu pamoja na hospitali ya kanda ya Magharibi unaotarajia kuanza 2024.

Kwa upande wake mkuu wa Wilaya ya Kigoma Hamis Kalli amesisitiza jamii kujenga utamaduni wa kufanya usafi ili kukabiliana na na athari zinazoweza kusababisha maradhi yanayoweza kusababishwa na uchafu. 

  • © Copyright - 2024
  • All rights reserved by - MainFm
  • Developed by - Mainfintech Lab