National News

MDAHALO WAFANYIKA KUELEKEA KILELE MAADHIMISHO SIKU YA UHURU KIGOMA

Tarehe: 09 Dec, 2023


Mkuu wa mkoa wa Kigoma Thobias Andengenye ameongoza Mdahalo
kuelekea Kilele cha Maadhimisho ya Miaka 62 ya Uhuru wa Tanzania Bara katika mkoa wa Kigoma uliolenga kuangazia na kubainisha mafanikio ambayo Mkoa pamoja na Taifa kwa Ujumla limeyapata tangu nchi ilipopata Uhuru.

Akifungua mdahalo huo, Andengenye amesema hatua za kimaendeleo zilizofikiwa tangu nchi kupata Uhuru ni jambo la kujivunia na inapaswa kuwa chachu katika kuzidi kusimamia vizuri miradi ya maendeleo inayotekelezwa na Serikali ya Awamu ya Sita.

Amesema ni muhimu kwa watanzania kutafakari na kufahamu mustakabali wa Taifa kwa lengo la kufahamu kuhusu  hali halisi ya maendeleo kabla na baada ya kupata Uhuru ili kujiwekea mipango endelevu ya kitaifa.

Akichangia mdahalo huo, Mganga Mkuu wa Mkoa wa Kigoma Dkt. Jesca Lebba amesema wakati nchi inapata Uhuru mkoa ulikuwa na watoa huduma za Afya chini ya mia moja ambapo kwa sasa waliopo kazini ni 2332 huku vituo vya kutolea huduma za Afya vilikuwa chini ya Kumi ambapo kwa sasa  vipo 307.

Ameendelea kueleza kupitia mdahalo huo kuwa, Mkoa umewezeshwa kutoa huduma  za X ray, uchunguzi wa Figo na kuongezeka kwa utolewaji wa Huduma nyingine za kibingwa kadhalika katika kufanikiwa  kupunguza kasi ya kuenea kwa virusi vya UKIMWI kutoka  Asilimia 2.9 hadi 1.7.

Upande wake mwakilisha mada kwa niaba ya Afisa Elimu Mkoa wa Kigoma, Mwalimu Shukurani Kalegamye amesema wakati nchi inapata Uhuru mkoa ulikuwa na shule mbili za Sekondari na Shule za msingi 73 ambapo mpaka kufikia mwaka 2023 mkoa una jumla ya Shule za Sekondari 237 na za msingi 722.
..........................
Tufuatilie zaidi kupitia
www.mainfm.co.tz
#instagram @mainfmtanzania
#facebook @mainfmtanzania
#twitter @mainfmtanzania

  • © Copyright - 2024
  • All rights reserved by - MainFm
  • Developed by - Mainfintech Lab