National News

VIONGOZI MBALIMBALI WA SERIKALI WAENDELEA KUWASILI HANANG

Tarehe: 04 Dec, 2023


Viongozi mbalimbali akiwemo Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera Bunge na Uratibu)  Jenista Mhagama na Waziri wa Ujenzi Innocent Bashungwa, pamoja na Wakuu wa Vyombo vya ulinzi na Usalama leo tarehe 04 Disemba 2023 wamefika katika kijiji cha Gendabi kata ya Gendambi Wilaya ya Hanang mkoani Manyara eneo yalipotokea mafuriko ambayo yamesababisha vifo vya watu, majeruhi na uharibifu mkubwa wa Miundombinu mbalimbali, yakiwamo mashamba na makazi ya wananchi. 

Katika ziara hiyo viongozi hao wameongozwa na Mkuu wa Mkoa Manyara, Queen Sendiga kufika katika Kijiji hicho eneo ambalo limeathirika kwa kiasi kikubwa na Maporomoko ya Matope kutoka Mlima wa Hanang yaliyotokea usiku wa kuamkia tarehe 03 Disemba mwaka huu. 

Aidha, Waziri Mhagama amesema kuwa Serikali imeshapeleka wataalamu wa Miamba ambapo watatoa taarifa ya nini kilichotokea na nini kifanyike katika mlima wa Hanang

Kwa upande wake Waziri wa Ujenzi, Innocent Bashungwa amesema kazi ya kufungua miundombinu ya barabara inaendelea ili kurahisia kazi za uokoaji na kufikisha huduma muhimu za kijamii katika meneo yaliyoathirika.

Aidha ameongeza kuwa Wakala wa Barabara nchini ( TANROADS) tayari wamefungua Barabara ya Singida-Babati ambayo awali ilikuwa haipitiki kutokana na kujaa tope na magogo ya miti kutoka milimani.
.........................
Tufuatilie zaidi kupitia
www.mainfm.co.tz
#instagram @mainfmtanzania
#facebook @mainfmtanzania
#twitter @mainfmtanzania


  • © Copyright - 2024
  • All rights reserved by - MainFm
  • Developed by - Mainfintech Lab