National News

VITUO 93 VYA TIBA NA MAFUNZO KWA WANAOISHI NA VVU VIMEANZISHWA KIGOMA

Tarehe: 02 Dec, 2023


Mkuu wa wilaya ya Buhigwe kanali Michael Masala amesema kuwa serikali imefanikiwa kuanzisha vituo 93 kwa ajili ya kutoa tiba na mafunzo kwa wanaoishi na VVU ikiwa ni sawa na asilimia 97.9 ya mahitaji halisi ya mkoa wa Kigoma.

Kanali Masala ameyasema hayo katika kilele cha maadhimisho ya siku ya ukimwi duniani akimwakilisha mkuu wa mkoa wa Kigoma Thobias Andengenye yaliyofanyika kimkoa katika Kijiji cha Songambele wilaya ya Buhigwe.

Katika hatua nyingine Kanali Masala amewataka wananchi mkoani Kigoma kuendelea kuchukua tahadhari dhidi ya tatizo la kuongezeka uzito uliopitiliza Pamoja na kujenga tabia ya kupima Afya mara kwa mara ili kuwasaidia kubaini maradhi katika hatua za awali ikiwemo ugonjwa wa kisukari na shinikizo la damu.

Aidha akitoa taarifa ya hali ya utekelezaji wa afua mbalimbali za UKIMWI kimkoa kaimu mganga mkuu wa mkoa Kigoma Innocent Msilikale amesema kuwa kuanzia Januari hadi Oktoba mwaka huu jumla ya watu laki 409,785 wamepima VVU saw ana asilimia 0.93 ya waliopima.
..........................
Tufuatilie zaidi kupitia
www.mainfm.co.tz
#instagram @mainfmtanzania
#facebook @mainfmtanzania
#twitter @mainfmtanzania