National News

MWENYEKITI CCM TAIFA ARIDHIA OMBI LA KUJIUZULU KWA CHONGOLO

Tarehe: 29 Nov, 2023


Mwenyekiti wa CCM taifa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan ameridhia ombi la kujiuzulu kwa katibu mkuu wa chama hicho taifa Daniel Chongolo baada ya kupokea barua ya kujiuzulu kwake

Hayo yamesemwa na Katibu wa NEC, Itikadi, Uenezi wa CCM Taifa, Paul Makonda leo Jijini Dar es salaam wakati akitoa taarifa kuhusu Kikao cha kawaida cha Halmashauri Kuu ya CCM ya Taifa kilichoketi leo Jijini Dar es salaam chini ya Mwenyekiti na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan. 

Sambamba na hayo kikao hicho kimejadili hali ya kisiasa ndani ya Chama na nje ya Chama hicho nchini na kimefanya uteuzi wa mwisho wa Wagombea wa nafasi za uongozi ndani ya Chama kwa ngazi ya Mkoa na Wilaya ili kujaza nafasi zilizoachwa wazi kutokana na sababu mbalimbali ikiwemo kifo na uteuzi wa nafasi nyingine. 


  • © Copyright - 2024
  • All rights reserved by - MainFm
  • Developed by - Mainfintech Lab