VIONGOZI SERIKALI ZA MITAA WASISITIZWA KUZUIA MIGOGORO
Tarehe: 28 Nov, 2023
Watendaji wa Kata na Maafisa Tarafa wametakiwa kuhakikisha wanakuwa mstari wa mbele katika kuzuia migogoro kati ya Serikali na wananchi hasa migororo ya ardhi kwa kuwa mingi inaanzia kwenye ngazi zao.
Wito huo umetolewa na Mkuu wa mkoa wa Tabora Dkt. Batilda Buriani alipokuwa akifunga Mafunzo ya viongozi hao yaliyofanyika kwa siku mbili katika mkoa huo.
Amesema migogoro ya ardhi imekuwa ni changamoto kubwa katika maeneo mengi na kuwaelekeza maafisa hao kuwa wazalendo na imani na kutumia misingi ya haki na sio upendeleo pale linapokuja suala la uuzaji wa ardhi za watu.
"Baadhi ya vijiji wameuza ardhi na wananchi wanalalamika hii inasababisha baadae migogoro kati ya serikali na wananchi wake mnapaswa kuwa na maadili mnapotekeleza majukumu yenu,"- amesema.
Aidha, amesisitiza viongozi hao kuwa na ushirikiano mzuri na wananchi wanaowaongoza kwenye maeneo yao.