National News

WANANCHI WALIA NA KORONGO

Tarehe: 21 Nov, 2023


Baadhi ya wananchi katika mtaa wa Bushabani kata ya Kibirizi Manispaa ya Kigoma Ujiji Mkoani Kigoma wameiomba serikali kuwasaidia ili waondokane na kero ya korongo ambalo limekwa la muda mrefu na kusababisha athari kwa baadhi ya wakazi wa eneo hilo

Wakizungumza na Main fm kwa nyakati tofauti wananchi hao wamesema kuwa changamoto hiyo ni ya muda mrefu hali inayohatarisha usalama wao na Watoto huku wakibainisha kuwa wamekuwa wakiahidiwa kuhusu kutatuliwa kwa kero hiyo bila mafanikio 

Nae mmoja wa waathirika wa korongo hilo Bi. Amina Paulo amesema uwepo wa korongo hilo umesababisha kupoteza nyumba yake kutokana na mvua ambapo kwasasa amepata hifadhi kwa Jirani yake na kuomba kusaidiwa kutokana na changamoto hiyo

Kwa upande wake mwenyekiti wa mtaa huo Bw. Majaliwa Manga wakati akielezea kuhusiana na tukio hilo amesema kuwa tangu Novemba 1 mwaka huu mkandarasi alitakiwa kuwa ameanza kutengezeneza eneo hilo lakini mpaka sasa sababu za kutoanza ujenzi huo hazijulikani

  • © Copyright - 2024
  • All rights reserved by - MainFm
  • Developed by - Mainfintech Lab