National News

WOSIA UNASAIDIA KUPUNGUZA VURUGU KATIKA FAMILIA-WAKILI KIVILO

Tarehe: 24 Jul, 2023


Imeelezwa kuwa kuna umuhimu mkubwa wa kuandika wosia kabla ya kufariki ili kuondoa mivutano mbalimbali inayoweza kujitokeza katika familia na kuleta madhara

Hayo yamesemwa na wakili na Mwenyekiti wa chama cha Mawakili mkoa wa Kigoma Eliuta Kivilo wakati wa mahojiano na Main fm na kuongeza kuwa kuandika wosia kunatoa utaratibu mzuri wa usimamizi wa mali na kuondoa migogoro kutokana na vurugu zinazoweza kujitokeza baada ya mhusika kufariki

Pia wakili huyo ameongeza kuwa hakuna uhusiano wowote kati ya kifo na wosia kutokana na baadhi ya watu kuamini kuwa unapoandika wosia unajitabilia kifo bali ni kutengeneza utaratibu mzuri utakaowaongoza baada ya mhusika kufariki

Aidha wakili huyo ameongeza kuwa kwa mkoa wa Kigoma kumekuwa na mwitikio mdogo wa watu kuandika wosia kutoakana na uelewa mdogo kuhusu jambo hilo

  • © Copyright - 2024
  • All rights reserved by - MainFm
  • Developed by - Mainfintech Lab