National News

SILAA AKUTANA NA WATENDAJI IDARA YA ARDHI KIGOMA

Tarehe: 16 Nov, 2023


Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Jerry Slaa amekutana na kufanya Kikao kazi na watendaji wa Serikali, Idara ya Ardhi mkoani Kigoma kwa lengo la kufuatilia utekelezaji wa Maamuzi ya Baraza la Mawaziri kuhusu utatuzi wa Migogoro ya Ardhi katika vijiji 975 vya Tanzania bara.

Kupitia kikao hicho Waziri Slaa amesisitiza watendaji hao kuongeza kasi katika kutatua migogoro hiyo pamoja na uwepo wa changamoto mbalimbali za kiutendaji kazi.

Aidha Waziri Slaa amewapongeza watendaji hao kwa kazi nzuri wanayoendelea kuifanya katika utekelezaji wa miradi mbalimbali ya Serikali kwa lengo la kuwaletea maendeleo wananchi.

Awali akitoa Salamu za ukaribisho kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Kigoma, Mkuu wa Wilaya ya Buhigwe  Kanali Michael Masala amesema Mkoa wa Kigoma ni miongoni mwa mikoa inayoguswa na maagizo ya Baraza la Mawaziri ikiwemo  kuondolewa kwa baadhi ya vijiji katika maeneo tengefu ya hifadhi za wanyama na mapori ya akiba.

Amesema mkoa unaendelea kuchukua hatua mbalimbali katika kutekeleza maagizo ya baraza la mawaziri kwa lengo la kuwaondolea wananchi kero zitokanazo na migogoro ya Ardhi.

Aidha amemshukuru Rais Dkt. Samia Suluhu kwa jitihada zake za kuwaletea maendeleo wananchi wa mkoa wa Kigoma na Tanzania kwa ujumla.
cc:kigomars 
..........................
Tufuatilie zaidi kupitia
#instagram @mainfmtanzania
#facebook @mainfmtanzania
#twitter @mainfmtanzania

  • © Copyright - 2024
  • All rights reserved by - MainFm
  • Developed by - Mainfintech Lab