Sports

"MGENI RASMI KATIKA MCHEZO WA SIMBA NA ASEC NI MASHABIKI"- AHMED ALLY

Tarehe: 16 Nov, 2023


Meneja wa Habari na Mawasiliano wa Klabu ya Simba Ahmed Ally amesema katika mchezo wao dhidi ya Asec Mimosas wa hatua ya makundi wa ligi ya Mabingwa barani Afrika mgeni rasmi wa mchezo huo watakuwa ni mashabiki wa Klabu hiyo.

“Wageni rasmi wa mechi ya Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya ASEC Mimosas watakuwa ni mashabiki wa Simba. Kwanza wametoka kushinda tuzo ya mashabiki bora hivyo kila Mwanasimba akija siku hiyo ajue yeye ni mgeni rasmi.” - Ahmed Ally

Mchezo huo unatarajiwa kupigwa Novemba 25, 2023 jijini Dar es Salaam ambapo Simba atakuwa mwenyeji wa mchezo huo.
..........................
Tufuatilie zaidi kupitia
#instagram @mainfmtanzania
#facebook @mainfmtanzania
#twitter @mainfmtanzania

  • © Copyright - 2024
  • All rights reserved by - MainFm
  • Developed by - Mainfintech Lab