National News

ZIARA ANAZOFANYA RAIS SAMIA ZINALETA TIJA KATIKA UCHUMI- ULEGA

Tarehe: 15 Nov, 2023


#Habari: Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Abdallah Ulega amesema kuwa ziara anazofanya Rais Samia Suluhu Hassan nje ya nchi zina tija kubwa kwa ustawi na maendeleo ya nchi.

Akizungumza na waandishi wa habari Ikulu jijini Dar es Salaam Ulega amesema dunia ya sasa haitaki watu kujifungia, bali inataka nchi kujitangaza na kuwaeleza wawekezaji kwanini wawekeze kwenye nchi husika au kwanini watalii watembelee nchi husika.

Amesisitiza kuwa Rais anapokuwa kwenye ziara nje, hufanya kazi muda wote akitangaza fursa mbalimbali zinazopatikana nchini.

Ametoa wito kwa waandishi wa habari kutumia nafasi zao kuwaeleza Watanzania manufaa ya ziara za Rais ili wasidhani kuwa anapokwenda katika nchi mbalimbali huenda kutembea, bali amekwenda kutafuta fursa kwa Watanzania na Tanzania kwa ujumla.
..........................
Tufuatilie zaidi kupitia
www.mainfm.co.tz
#instagram @mainfmtanzania
#facebook @mainfmtanzania
#twitter @mainfmtanzania

  • © Copyright - 2024
  • All rights reserved by - MainFm
  • Developed by - Mainfintech Lab