National News

WHOZU, MBOSO NA BILNASS WATAKIWA KULIPA FAINI ILI WAENDELEE NA KAZI YAO YA MUZIKI

Tarehe: 14 Nov, 2023


#Burudani: Baada ya kufungiwa kwa wasanii Whozu, Mbosso na Bilnass baada ya kutoa video ya wimbo wa "AMEYATIMBA"  hatimaye kikao cha kusikiliza rufaa ya Wanamuziki hao kimefanyika leo ambacho kimefikia maamuzi ya kuwataka wasani hao kulipa faini ili waweze kuruhusiwa kufanya kazi za sanaa nchini kwa kufuata maadili ya Kitanzania.

Maamuzi hayo yamefikiwa kwenye kikao chini ya uongozi wa Waziri wa Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Dkt. Damas Ndumbaro kilichofanyika uwanja wa Benjamini Mkapa jijini Dares salaam ambapo Mwanamuziki Whozu anatakiwa kulipa faini huku Bilnass na Mbosso wakiondolewa adhabu za kufungiwa.

Mhe. Waziri amewahasa wasani hao na wengine nchini kutumia ubunifu kwa kufuata taratibu ulioainishwa katika muongozo wa uzingatiaji maadili katika kazi za sanaa.

Whozu amepewa masaa sita ili kutekeleza azimio la kushusha wimbo huo kwenye Digital platforms zote kama makubaliano yanavyoelekeza.
..........................
Tufuatilie zaidi kupitia
www.mainfm.co.tz
#instagram @mainfmtanzania
#facebook @mainfmtanzania
#twitter @mainfmtanzania

  • © Copyright - 2024
  • All rights reserved by - MainFm
  • Developed by - Mainfintech Lab