National News

SERIKALI YAONYA WANAOWASHAMBULIA WAANDISHI WA HABARI

Tarehe: 13 Nov, 2023


Serikali imekemea vikali matendo maovu yanayofanywa na baadhi ya watu ya kuwashambulia waandishi wa Habari wanapokuwa katika utekelezaji wa majukumu yao.

Kauli hiyo imetolewa na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Kassim Majaliwa leo  Novemba 13, 2023 katika uwanja wa Ilulu mkoani Lindi katika mkutano mkuu 7 wa mwaka wa Jukwaa la Wahariri (TEF).

“Suala la usalama wa wanahabari limezungumzwa sana na tunaendelea kulitolea ufafanuzi. Nianze kwa kutoa pole kwa wanahabari wote waliokumbwa na changamoto hii ya kuguswa kwenye harakati za usalama; iwe umeshambuliwa ukiwa kazini, au umepata tatizo ukielekea mahali pa kazi, kimsingi vitendo hivi havikubaliki. Serikali tumeshatoa taarifa kwa vyombo vyetu kuzingatia umuhimu wa uwepo wa wanahabari kwenye matukio yetu.” – Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa
..........................
Tufuatilie zaidi kupitia
www.mainfm.co.tz
#instagram @mainfmtanzania
#facebook @mainfmtanzania
#twitter @mainfmtanzania

  • © Copyright - 2024
  • All rights reserved by - MainFm
  • Developed by - Mainfintech Lab