Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk.Hussein Ali Mwinyi ameushukuru uongozi wa klabu ya Yanga kwa kuipeleka timu ya mpira wa miguu ya Kaizer Chiefs kutoka Afrika Kusini kutalii Visiwani humo.
Dkt.Mwinyi ameyasema hayo alipokutana na Viongozi na Wachezaji kutoka Timu ya Kaizer Chiefs ya Afrika Kusini waliofika Ikulu Zanzibar na kuongeza kuwa Zanzibar ni nchi ya utalii ikiwemo utalii wa fukwe za bahari na mji mkongwe ambapo ameeleza kuwa kufika kwa Kaizer Chiefs ni fursa ya kuitangaza Zanzibar zaidi Afrika ya Kusini na kimataifa kupitia utalii wa michezo ambayo ni ndoto yake ya muda mrefu.
Kwa upande wake Rais wa Timu ya Yanga Injinia Hersi Ally Said amesema kwa juhudi zinazofanywa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Hussein Ali Mwinyi katika kukuza utalii wameamua kumuunga mkono kwa kuwaleta Timu ya Kaizer Chiefs yenye historia barani Afrika wafike Zanzibar kutalii na kuitangaza Zanzibar kimataifa zaidi.