National News

PELEKENI AMBULANCE SEHEMU ZENYE UHITAJI- DKT. TULIA

Tarehe: 11 Nov, 2023


#Habari: Spika wa Bunge Dkt. Tulia Ackson amekabidhi magari ya dharura ya kubebea wagonjwa (Ambulance) 49 kwa wabunge kati ya magari 528 yaliyotolewa na Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa wabunge wa majimbo yote nchini.

Akikabidhi magari hayo, Dkt. Tulia amewataka wabunge hao kuyapeleka magari hayo kwenye maeneo yenye uhitaji mkubwa bila kuangalia urafiki au chuki na Wakurugenzi. 

"Tunaposema Rais Samia anaupiga mwingi tunamaanisha kazi kama hizi anazofanya, magari haya ni jitihada zake hivyo lazima tuunganisha mafanikio haya na jitihada za Rais ameendelea kujali watanzania hasa katika upande wa afya kwa kweli tunamshukuru sana."

"Pelekeni magari haya katika maeneo yenye tija kama alivyokusudia Mheshimiwa Rais Samia ili kuendelea kuboresha huduma za afya kwa watanzania,"amesema Dkt. Tulia.
cc: ortamisemi
..........................
Tufuatilie zaidi kupitia
www.mainfm.co.tz
#instagram @mainfmtanzania
#facebook @mainfmtanzania
#twitter @mainfmtanzania