National News

MAKONDA AIAGIZA TAKUKURU KUCHUNGUZA VIASHIRIA VYA RUSHWA WILAYA YA MULEBA

Tarehe: 10 Nov, 2023


Katibu wa Itikadi, Uenezi na Mafunzo wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Paul Makonda, amewaagiza taasisi ya kuzuia na kupambana na Rushwa Tanzania TAKUKURU kuchunguza viashiria vya Rushwa katika Wilaya ya Muleba mara baada yakusema kuna viashiria vya harufu ya rushwa katika eneo hilo.

Makonda ameyasema hayo akiwa njiani kuelekea Chato kuzuru kaburi la Hayati Dkt. John Pombe Magufuli ambapo amesema amepata malalamiko ya wananchi kuhusu vitendo hivyo na yeye akiwa ni msaidizi wa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan hawezi kuacha wananchi kuonewa na baadhi ya watendaji wasio waaminifu na kudhurumu haki za wanyonge.

Katika hatua nyingine Makonda amewaahidi wananchi akifika kaburini kwa Hayati Magufuli ataongea nae na kumwambia mema yanayoendelea kufanywa na mrithi wake Dkt. Samia kwakua mengi yaliyoachwa yanaendelea ikiwa ni pamoja na mikopo ya wanafunzi wa elimu wa juu, huduma za maji, nishati na miundombinu ya barabara.
..........................
Tufuatilie zaidi kupitia
www.mainfm.co.tz
#instagram @mainfmtanzania
#facebook @mainfmtanzania
#twitter @mainfmtanzania

  • © Copyright - 2024
  • All rights reserved by - MainFm
  • Developed by - Mainfintech Lab