National News

ALIYEKUWA MKURUGENZI IGUNGA AFIKISHWA MAHAKAMANI NA WENZAKE 10

Tarehe: 08 Nov, 2023


Aliyekuwa Mkurugenzi wa  Halmashauri ya Wilaya ya Igunga Mkoani Tabora Athumani Msabila na watumishi kumi wa Umma, wamefikishwa katika Mahakama ya Wilaya ya Kigoma na kusomewa Mashtaka mbalimbali ikiwemo uhujumu uchumi.

Washitakiwa hao wamesomewa Mashtaka hayo mnamo Novemba 7, 2023 na wakili Mwandamizi wa Serikali Anasisye Erasto mbele ya Hakimu Mkazi wa Mahakama hiyo Hassan Momba.

Akisoma Hati ya Mashtaka wakili Anasisye amesema washtakiwa hao wanakabiliwa na makosa 11 waliyoyatenda nyakati mbalimba  katika Mkoa wa Kigoma na Dodoma ikiwemo kuisababishia Serikali hasara, kugushi nyaraka za serikali, matumizi mabaya ya ofisi pamoja na kukiuka haki na maslahi ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Aidha washtakiwa hao hawakutakiwa kujibu mashtaka yao  na wamerudishwa rumande mpaka  kesi inayowahusu itakapotajwa tena.
..........................
Tufuatilie zaidi kupitia
www.mainfm.co.tz
#instagram @mainfmtanzania
#facebook @mainfmtanzania
#twitter @mainfmtanzania

  • © Copyright - 2024
  • All rights reserved by - MainFm
  • Developed by - Mainfintech Lab