National News

WIMBO WA "AMEYATIMBA" WAMPONZA WHOZU AFUNGIWA MIEZI 6 KUTOJIHUSISHA NA MUZIKI

Tarehe: 05 Nov, 2023


Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) limemtaka Msanii Whozu kushusha mara moja video ya wimbo wake wa ‘Ameyatimba’ kwenye mitandao yote, pia limemtoza faini ya Tsh. milioni 3 na limemfungia kujishughulisha na kazi za sanaa kwa muda wa miezi 6 kuanzia November 04, 2023 kutokana na wimbo huo kuwa na maudhui yanayokiuka kanuni za maadili.

Wimbo huo una maudhui yanayokiuka kanuni za maadili kutokana na kuwepo ishara ya vitendo vinavyoashiria matusi kinyume na Kanuni ya 25(6) (j) pamoja na vitendo vya unyanyasaji, ukatili na udhalilisha wa utu wa Mwanamke kinyume na Kanuni ya 25(6)-(f).

Pia BASATA imewafungia Wasanii Mbosso na Billnas kutokujishughulisha na kazi za sanaa kwa muda wa miezi mitatu kuanzia November 04, 2023 kutokana na Wasanii hao kushirikishwa kwenye wimbo huo wa ‘Ameyatimba’ huku likiwatoza faini ya milioni tatu kila mmoja
..........................
Tufuatilie zaidi kupitia
www.mainfm.co.tz
#instagram @mainfmtanzania
#facebook @mainfmtanzania
#twitter @mainfmtanzania

  • © Copyright - 2024
  • All rights reserved by - MainFm
  • Developed by - Mainfintech Lab