National News

"KIGOMA SIYO MKOA WA WATENDAJI WALIOFANYA VIBAYA"-NG'ENDA

Tarehe: 04 Nov, 2023


Mbunge wa Kigoma mjini (CCM) Shabani Kilumbe Ng'enda amesema Kigoma inarudishwa nyuma kimaendeleo kwa sababu ni mkoa unaochukuliwa kama sehemu ya kuwaadhibu watumishi wanaokosea.

Akizungumza Bungeni Novemba 3, 2023 Ng'enda alisema kila mtumishi anayefanya makosa eneo moja anapelekwa Kigoma kama sehemu ya adhabu kwa mtumishi huyo.

"Huu mfumo wa kufanya halmashauri zetu zisiwe na uwezo umetengenezwa, suala la halmashauri kuwa na uwezo ni mzunguko wa fedha wa wananchi wenyewe, kama hao wananchi umewanyima treni, meli, viwanda na kila mfanyakazi anayefanya makosa mahala unampeleka Kigoma kama adhabu, unaugeuza mkoa kuwa guantanamo ya watu kuadhibiwa, unategemea nini?" - Amesema Ng'enda

Ameongeza kuwa halmashauri za mkoa wa Kigoma haziwezi kuonekana zikifanya vizuri katika makusanyo ya fedha kwa ajili ya maendeleo ya mkoa huo kama unatumika kama mkoa wa adhabu kwa wafanyakazi.

"Aliyeiba huko mkaona hafanyi vizuri peleka Kigoma, aliyekosa adabu eneo moja peleka Kigoma, kwamba Kigoma ni eneo la adhabu halafu unategemea wafanye vizuri, haiwezekani" - Ng'enda.
..........................
Tufuatilie zaidi kupitia
#instagram @mainfmtanzania
#facebook @mainfmtanzania
#twitter @mainfmtanzania

  • © Copyright - 2024
  • All rights reserved by - MainFm
  • Developed by - Mainfintech Lab