National News

BULAYA APENDEKEZA BALOZI SIRRO AREJESHWE NCHINI KUJA KUJIBIA UBADHILIFU FEDHA ZA MFUKO WA POLISI

Tarehe: 03 Nov, 2023


Mbunge wa Viti maalum Esther Bulaya amesema ipo haja ya Balozi Simon Sirro kurejeshwa nchini ili ajibie kuhusu ubadhirifu wa fedha katika mfuko wa polisi zilizotajwa katika ripoti ya CAG.

Akichangia mjadala wa uchambuzi wa Ripoti ya CAG, Bulaya amesema kwa mujibu wa Kifungu cha 66(3) cha Sheria ya Jeshi la Polisi Sura Na. 333 kimeainisha Mkuu wa Jeshi la Polisi (IGP) ndiye mwenye mamlaka ya matumizi ya Fedha za Mfuko huo ambapo hadi Ukaguzi unafanywa Balozi Simon Sirro alikuwa IGP.

Amesema ukaguzi umeonesha kulikuwa na ubadhirifu wa takriban Tsh. Bilioni 1, hivyo Serikali imrudishe Balozi Sirro kuja kueleza kilichotokea kwasababu Mfuko huo ulianzishwa kwa lengo la kuwasaidia Askari wanapopatwa na matatizo kazini.
..........................
Tufuatilie zaidi kupitia
#instagram @mainfmtanzania
#facebook @mainfmtanzania
#twitter @mainfmtanzania

  • © Copyright - 2024
  • All rights reserved by - MainFm
  • Developed by - Mainfintech Lab