National News

DC KIGOMA ASISITIZA CHAKULA MASHULENI NA KUFANYA MAZOEZI YA VIUNGO

Tarehe: 03 Nov, 2023


Mkuu wa Wilaya ya Kigoma Ndugu. Salum Hamis Kali amewataka Watendaji Kata na Mitaa kuendelea kuhamasisha Wazazi, Walezi na Wadau mbalimbali kutoa chakula  shuleni.
  
Aliyasema hayo alipokuwa akifungua kikao cha tathimini ya utekelezaji wa viashiria vya Mkataba wa lishe baina ya Mkurugenzi wa Manispaa ya Kigoma /ujiji na Watendaji Kata kilichofanyika  katika Ukumbi wa Manispaa hiyo.

Aliwataka Watendaji Kata kufanya Vikao na Mikutano ya Wazazi, Walezi na Wadau mbalimbali kuweka mikakati ya kufanikisha upatikanaji wa Chakula wakati wa masomo kwa lengo la kupandisha viwango vya ufaulu. 

Mkuu huyo wa Wilaya alisisitiza Suala la Mazoezi kwa wakazi wa Manispaa hiyo huku akitoa ratiba yake ya Mazoezi ya Kushiriki na Wananchi ikiwa ni Kila Siku ya Jumatano Saa kumi na nusu (16:30) Jioni Uwanja wa Mwanga Community Centre na kila Siku ya Jumamosi Saa kumi na mbili asubuhi yakianzia eneo la stesheni. 

Aidha amewataka Watendaji Kata kuendelea kusimamia viashiria vya Mkataba kwa kuwasimamia wahudumu wa afya ngazi ya Jamii kuwasilisha taarifa kila Mwezi.

Awali akimkaribisha Mkuu wa Wilaya ya Kigoma, Mkurugenzi wa Manispaa ya Kigoma/Ujiji @mgonjamwantum Bi. Mwantum Mgonja alisema lengo la kikao hicho ni kujadili na  Kuboresha masuala ya lishe na kupunguza utapiamlo kwa Wakazi wa Manispaa ya Kigoma/Ujiji

cc.kigomaujijimc