National News

DKT.MWINYI AISHUKURU YANGA KUIPELEKA KAIZER CHIEFS KUTALII ZANZIBAR

Tarehe: 23 Jul, 2023


Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk.Hussein Ali Mwinyi ameushukuru uongozi wa klabu ya Yanga kwa kuipeleka timu ya mpira wa miguu ya Kaizer Chiefs kutoka  Afrika Kusini  kutalii Visiwani humo.

Dkt.Mwinyi ameyasema hayo alipokutana na Viongozi na Wachezaji kutoka Timu ya Kaizer Chiefs ya Afrika Kusini waliofika  Ikulu Zanzibar na kuongeza kuwa Zanzibar ni nchi ya  utalii  ikiwemo utalii wa fukwe za bahari na mji mkongwe ambapo ameeleza kuwa  kufika kwa   Kaizer Chiefs  ni fursa ya kuitangaza Zanzibar  zaidi  Afrika ya  Kusini na kimataifa  kupitia utalii wa michezo ambayo ni ndoto yake ya muda mrefu.  

Kwa upande wake Rais wa Timu ya Yanga Injinia Hersi Ally Said amesema kwa juhudi zinazofanywa  na  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Hussein Ali Mwinyi katika  kukuza utalii wameamua kumuunga mkono kwa kuwaleta Timu ya Kaizer Chiefs yenye historia barani Afrika wafike  Zanzibar kutalii  na kuitangaza Zanzibar kimataifa zaidi.

  • © Copyright - 2024
  • All rights reserved by - MainFm
  • Developed by - Mainfintech Lab