National News

"KAMCHAPE HAIKUKUBALIKI"-ACP KIYOGOMO

Tarehe: 20 Jul, 2023


  • Jeshi la polisi mkoani Kigoma limeonya kuhusu vitendo vinavyofanywa na waganga wa kienyeji maarufu kama "Lambalamba/Kamchape"na kusema kuwa havikubaliki huku likiwataka wote wanaojihusisha na vitendo hivyo kuacha maramoja kwasababu ni chanzo kikubwa cha matatizo mbalimbali katika jamii ikiwemo Migogoro na uchonganishi.

  • Kauli hiyo imetolewa na Kamishina Msaidizi wa Polisi mkoani  Kigoma ACP Iddy Kiyogomo wakati wa mahojiano na Main fm na kusema kuwa jeshi hilo litaendelea kufuatilia katika maeneo yanayoendelea na matukio hayo.

  • KamandaKiyogomo ameongeza kuwa katika kipindi ambacho operesheni ya kuwakamata Lambalamba/ Kamchape wamefanikiwa kuwakamata watu kadhaa wakiwemo waganga wanaojihusisha na matukio hayo ambapo waathirika wengi katika matukio hayo ni wanawake.

  • Kamanda huyo amewasihi wananchi kuendelea kutoa ushirikiano katika kutoa taarifa kuhusu vitendo mbalimbali mbalimbali vya kihalifu katika maeneo yao
  • ..............
  • Tufuatilie zaidi
  • Instagram @mainfmtanzania
  • Facebook @mainfmtanzania 
  • Twitter @mainfmtanzania

  • © Copyright - 2024
  • All rights reserved by - MainFm
  • Developed by - Mainfintech Lab